1Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”
2Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini,
3lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ”
4Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa.