22Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne.
23Mwana wa Dani ni: Hushimu.
24Wana wa Naftali ni: Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu.
25Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba.
26Wote waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe zake, walikuwa watu sitini na sita.