27Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.
28Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
29Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.”
30Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
31Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.