14kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.
15Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema:
16“Hili ndilo Agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.”
17Kisha aongeza kusema: “Dhambi zao na kutokutii kwao sitakumbuka tena.”
18Basi haya yakiisha kusamehewa, hakuna tena dhabihu yoyote inayotolewa kwa ajili ya dhambi.