12Vivyo hivyo, Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe.
13Kwa hiyo, basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba.
14Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao.
15Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.
16Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.