22majoho mazuri, mitandio, mavazi, kifuko cha kutilia fedha,
23vioo, mavazi ya kitani, taji na shali.
24Badala ya harufu ya manukato kutakuwa na uvundo; badala ya mishipi, ni kamba; badala ya nywele zilizotengenezwa vizuri, ni upara; badala ya mavazi mazuri, ni nguo za magunia; badala ya uzuri, ni alama ya aibu kwa chuma cha moto.
25Wanaume wako watauawa kwa upanga, nao mashujaa wako watauawa vitani.
26Malango ya Sayuni yataomboleza na kulia, ataketi mavumbini akiwa fukara.