Isaya 5

wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo, lakini huwanyima haki wasio na hatia.

Isaiah 5:23 (UKJV) Which justify the wicked for reward, and take away the righteousness of the righteous from him!

21Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe, na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe.

22Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo, nao walio hodari katika kuchanganya vileo,

23wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo, lakini huwanyima haki wasio na hatia.

24Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi, na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.

25Kwa hiyo hasira ya Bwana inawaka dhidi ya watu wake, mkono wake umeinuliwa na anawapiga. Milima inatetemeka, maiti ni kama takataka kwenye barabara. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.