Isaya 8

Funga ushuhuda na kutia muhuri sheria miongoni mwa wanafunzi wangu.

Isaiah 8:16 (UKJV) Bind up the testimony, seal the law among my disciples.

14naye atakuwa mahali patakatifu; lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa na mwamba wa kuwaangusha. Kwa watu wa Yerusalemu, atakuwa mtego na tanzi.

15Wengi wao watajikwaa; wataanguka na kuvunjika, watategwa na kunaswa.”

16Funga ushuhuda na kutia muhuri sheria miongoni mwa wanafunzi wangu.

17Nitamngojea Bwana, ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake. Nitaliweka tumaini langu kwake.

18Niko hapa, pamoja na watoto ambao Bwana amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.