Yeremia 37

Kisha Wakaldayo watarudi na kushambulia mji huu, watauteka na kuuchoma moto.’

Jeremiah 37:8 (UKJV) And the Chaldeans shall come again, and fight against this city, and take it, and burn it with fire.

6Ndipo neno la Bwana likamjia nabii Yeremia kusema:

7“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Mwambie mfalme wa Yuda aliyekutuma uniulize mimi, ‘Jeshi la Farao lililotoka kuja kukusaidia litarudi katika nchi yake yenyewe, yaani Misri.

8Kisha Wakaldayo watarudi na kushambulia mji huu, watauteka na kuuchoma moto.’

9“Hili ndilo Bwana asemalo: Msijidanganye wenyewe mkifikiri, ‘Hakika Wakaldayo watatuacha na kwenda zao.’ Hakika hawatawaacha!

10Hata kama mngelishinda jeshi lote la Wakaldayo linalowashambulia ninyi, na wakawa ni watu waliojeruhiwa tu waliobaki kwenye mahema yao, wangetoka na kuuchoma mji huu moto.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.