Yeremia 7

Lakini tazama, mnatumainia maneno ya udanganyifu yasiyo na maana.

Jeremiah 7:8 (UKJV) Behold, all of you trust in lying words, that cannot profit.

6kama msipomwonea mgeni, yatima wala mjane, na kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, nanyi kama msipofuata miungu mingine kwa madhara yenu wenyewe,

7ndipo nitawaacha mkae mahali hapa, katika nchi niliyowapa baba zenu milele na milele.

8Lakini tazama, mnatumainia maneno ya udanganyifu yasiyo na maana.

9“ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo, na kufukiza uvumba kwa Baali, na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua,

10kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.” Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.