3Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?
4Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?
5Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, au miaka yako ni kama ile ya mtu,
6ili kwamba utafute makosa yangu na kuichunguza dhambi yangu;
7ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?