5Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, au miaka yako ni kama ile ya mtu,
6ili kwamba utafute makosa yangu na kuichunguza dhambi yangu;
7ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?
8“Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. Je, sasa utageuka na kuniangamiza?
9Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?