13“Hekima na nguvu ni vya Mungu; shauri na ufahamu ni vyake yeye.
14Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.
15Akizuia maji, huwa pana ukame; akiyaachia maji, huharibu nchi.
16Kwake kuna nguvu na ushindi; adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.
17Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.