4Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!
5Laiti wote mngenyamaza kimya! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.
6Sikieni sasa hoja yangu; sikilizeni kusihi kwangu.
7Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?
8Mtamwonyesha upendeleo? Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?