3Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu.
4Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!
5Laiti wote mngenyamaza kimya! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.
6Sikieni sasa hoja yangu; sikilizeni kusihi kwangu.
7Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?