Ayubu 13

Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu.

Job 13:3 (UKJV) Surely I would speak to the Almighty, and I desire to reason with God.

1“Macho yangu yameona hili lote, masikio yangu yamesikia na kulielewa.

2Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua; mimi si mtu duni kuliko ninyi.

3Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu.

4Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!

5Laiti wote mngenyamaza kimya! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.