14“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi, au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu?
15Kama Mungu hawaamini watakatifu wake, kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake,
16sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu, ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji!
17“Nisikilize mimi nami nitakueleza, acha nikuambie yale niliyoyaona,
18ambayo watu wenye hekima wameyanena, bila kuficha lolote walilopokea toka kwa baba zao