3Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa, kwa hotuba zisizo na maana?
4Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu na kuzuia ibada mbele za Mungu.
5Dhambi yako inasukuma kinywa chako, nawe umechagua ulimi wa hila.
6Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu; midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako.
7“Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? Ulizaliwa kabla ya vilima?