Ayubu 15

Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu na kuzuia ibada mbele za Mungu.

Job 15:4 (UKJV) Yea, you cast off fear, and restrain prayer before God.

2“Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu, au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki?

3Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa, kwa hotuba zisizo na maana?

4Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu na kuzuia ibada mbele za Mungu.

5Dhambi yako inasukuma kinywa chako, nawe umechagua ulimi wa hila.

6Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu; midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.