Ayubu 18

Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, na kuonekana wajinga machoni pako?

Job 18:3 (UKJV) Wherefore are we counted as beasts, and reputed vile in your sight?

1Bildadi Mshuhi akajibu:

2“Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea.

3Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, na kuonekana wajinga machoni pako?

4Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?

5“Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.