18Hata watoto wadogo hunidhihaki; ninapojitokeza, hunifanyia mzaha.
19Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa; wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.
20Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu; nimeponea nikiwa karibu kufa.
21“Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma, kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga.
22Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo? Hamtosheki kamwe na mwili wangu?