Ayubu 19

Kama ni kweli nimepotoka, kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe.

Job 19:4 (UKJV) And be it indeed that I have erred, mine error remains with myself.

2“Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini, na kuniponda kwa maneno yenu?

3Mara kumi hizi mmenishutumu; bila aibu mnanishambulia.

4Kama ni kweli nimepotoka, kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe.

5Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu, na kutumia unyonge wangu dhidi yangu,

6basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya, naye amekokota wavu wake kunizunguka.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.