7“Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu; ingawa ninaomba msaada, hakuna haki.
8Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita; ameyafunika mapito yangu na giza.
9Amenivua heshima yangu, na kuniondolea taji kichwani pangu.
10Amenibomoa kila upande hadi nimeisha; amelingʼoa tegemeo langu kama mti.
11Hasira yake imewaka juu yangu; amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake.