16Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.
17Hatafurahia vijito, mito inayotiririsha asali na siagi.
18Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.
19Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu; amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga.
20“Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana; hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.