6Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa, nao mwili wangu unatetemeka.
7Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu?
8Huwaona watoto wao wakithibitika wakiwa wamewazunguka, wazao wao mbele za macho yao.
9Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu; fimbo ya Mungu haiko juu yao.
10Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe; ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba.