15Je, utaifuata njia ya zamani, ambayo watu waovu waliikanyaga?
16Waliondolewa kabla ya wakati wao, misingi yao ikachukuliwa na mafuriko.
17Walimwambia Mungu, ‘Tuache sisi! Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?’
18Lakini ndiye alizijaza nyumba zao na vitu vizuri, hivyo ninajitenga mbali na mashauri ya waovu.
19“Wenye haki wanaona maangamizi yao na kufurahi, nao wasio na hatia huwadhihaki, wakisema,