5Je, uovu wako si mkuu? Dhambi zako si hazina mwisho?
6Umedai dhamana kwa ndugu zako bila sababu; umewavua watu nguo zao, ukawaacha uchi.
7Hukumpa maji aliyechoka, nawe ulimnyima chakula mwenye njaa,
8ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi: mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake.
9Umewafukuza wajane mikono mitupu na kuzivunja nguvu za yatima.