13“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga? Yeye hufanya lolote atakalo.
14Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu, na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba.
15Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake; nifikiriapo haya yote ninamwogopa.
16Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia; yeye Mwenyezi amenitia hofu.
17Hata hivyo sijanyamazishwa na giza, wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.