Ayubu 28

Ardhi, ambako chakula hutoka, chini hugeuzwa kwa moto;

Job 28:5 (UKJV) As for the earth, out of it comes bread: and under it is turned up as it were fire.

3Mwanadamu hukomesha giza; huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini katika giza jeusi sana.

4Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba.

5Ardhi, ambako chakula hutoka, chini hugeuzwa kwa moto;

6yakuti samawi hutoka katika miamba yake, nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu.

7Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, wala hakuna jicho la mwewe lililoiona.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.