1Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
2“Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita, zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda,
3wakati taa yake iliniangazia kichwani changu, na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza!
4Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu, wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu,
5wakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami, nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka,