10kwa sababu huo usiku haukunifungia mlango wa tumbo la mama yangu, ili kuyaficha macho yangu kutokana na taabu.
11“Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa? Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni?
12Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea na matiti ili nipate kunyonyeshwa?
13Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani. Ningekuwa nimelala na kupumzika
14pamoja na wafalme na washauri wa dunia, waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu,