12Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea na matiti ili nipate kunyonyeshwa?
13Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani. Ningekuwa nimelala na kupumzika
14pamoja na wafalme na washauri wa dunia, waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu,
15pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu, waliozijaza nyumba zao kwa fedha.
16Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu, kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga?