23Kwa nini uhai hupewa mtu ambaye njia yake imefichika, ambaye Mungu amemzungushia boma?
24Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula; kusononeka kwangu kunamwagika kama maji.
25Lile nililokuwa naliogopa limenijia; lile nililokuwa ninalihofia limenipata.
26Sina amani, wala utulivu; sina pumziko, bali taabu tu.”