20“Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu; ninasimama, nawe unanitazama tu.
21Wewe unanigeukia bila huruma; unanishambulia kwa nguvu za mkono wako.
22Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali.
23Ninajua utanileta mpaka kifoni, mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa.
24“Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji, anapoomba msaada katika shida yake.