19Yeye amenitupa kwenye matope, nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20“Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu; ninasimama, nawe unanitazama tu.
21Wewe unanigeukia bila huruma; unanishambulia kwa nguvu za mkono wako.
22Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali.
23Ninajua utanileta mpaka kifoni, mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa.