Ayubu 33

anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo,

Job 33:16 (UKJV) Then he opens the ears of men, and seals their instruction,

14Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe.

15Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao,

16anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo,

17ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi,

18kuiokoa nafsi yake na shimo, uhai wake usiangamizwe kwa upanga.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.