34“Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji?
35Je, wewe hutuma umeme wa radi kwenye njia zake? Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’?
36Ni nani aliyeujalia moyo hekima au kuzipa akili ufahamu?
37Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu? Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni
38wakati mavumbi yawapo magumu, na mabonge ya udongo kushikamana pamoja?