37Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu? Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni
38wakati mavumbi yawapo magumu, na mabonge ya udongo kushikamana pamoja?
39“Je, utamwindia simba jike mawindo, na kuwashibisha simba wenye njaa
40wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao, au wakivizia kichakani?
41Ni nani ampaye kunguru chakula wakati makinda yake yanamlilia Mungu, yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?