5Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? Hakika wewe unajua! Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?
6Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini, au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,
7wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?
8“Ni nani aliyeifungia bahari milango ilipopasuka kutoka tumbo,
9nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, na kuyafungia katika giza nene,