20Je, wewe humfanya farasi aruke kama nzige, akistaajabisha kwa tishio la mlio wake wa majivuno?
21Huparapara bila woga, akizifurahia nguvu zake, husonga mbele kukabiliana na silaha.
22Huicheka hofu, haogopi chochote, wala haukimbii upanga.
23Podo hutoa sauti kando yake, pamoja na mkuki unaongʼaa na fumo.
24Bila woga na kwa ghadhabu huimeza nchi, wala tarumbeta iliapo yeye hawezi kusimama.