18Mifupa yake ni bomba za shaba, maungo yake ni kama fito za chuma.
19Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu, lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.
20Vilima humletea yeye mazao yake, nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.
21Hulala chini ya mimea ya yungiyungi, katika maficho ya matete kwenye matope.
22Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake; miti mirefu karibu na kijito humzunguka.