5Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi,
6ikiwa wewe ni safi na mnyofu, hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, na kukurudisha katika mahali pako pa haki.
7Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo, lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.
8“Ukaulize vizazi vilivyotangulia na uone baba zao walijifunza nini,
9kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote, nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.