15Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu; ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie.
16Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali, siamini kama angenisikiliza.
17Yeye angeniangamiza kwa dhoruba na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.
18Asingeniacha nipumue bali angenifunika kabisa na huzuni kuu.
19Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu! Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?