Yoeli 3

Yuda itakaliwa na watu milele na Yerusalemu itadumu vizazi vyote.

Joel 3:20 (UKJV) But Judah shall dwell for ever, and Jerusalem from generation to generation.

18“Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa; mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji. Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya Bwana na kunywesha Bonde la Shitimu.

19Lakini Misri itakuwa ukiwa, Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda, ambao katika nchi yao walimwaga damu isiyo na hatia.

20Yuda itakaliwa na watu milele na Yerusalemu itadumu vizazi vyote.

21Hatia yao ya damu, ambayo sijasamehe, nitasamehe.” Bwana anakaa Sayuni!

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.