24Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo
25wakamuuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?”
26Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua.
27Yeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.”
28Mambo haya yote yalitukia huko Bethania, ngʼambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza.