17Yesu alipowasili huko alikuta Lazaro amekuwa kaburini siku nne.
18Basi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu umbali wa karibu maili mbili,
19na Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Maria kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao.
20Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Maria alibaki nyumbani.
21Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.