30Yesu akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu.
31Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.
32Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.”
33Yesu aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa.
34Ule umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka Sheria kwamba ‘Kristo adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”