Yohana 14

“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.

John 14:15 (UKJV) If all of you love me, keep my commandments.

13Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana.

14Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya.

15“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.

16Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele.

17Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.