14Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya.
15“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.
16Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele.
17Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.
18Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu.