Yohana 15

Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi.

John 15:3 (UKJV) Now all of you are clean through the word which I have spoken unto you.

1“Mimi ndimi mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima.

2Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi.

3Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi.

4Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda.

5“Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.